Tanzania! Tanzania!
Nchi yangu naipenda
Kuwa mtanzania ninafurahia
Kiswahili lugha yetu ndio
Yatuunganisha
Amani fahari yetu ndio
Yatupatanisha
Ninajivunia mimi kuwa mtanzania
Na kiswahili changu ndio ninaringia.
Mimi ni mtanzania
Nchi yangu naishangilia!
Kila sifa imejaaliwa
Upendo, mshikamano, ndio nguzo yetu kuu
Natembea kifua mbele
Popote niandapo macho huku na huku
Kwasababu najivunia mimi kuwa mtanzania
Na kiwsahili changu ndio ninaringia.
Tangu enzi na enzi kiswahili umoja wetu
Mbali kimetutoa kikaleta uhuru wetu
Nasema ahsante Mungu
Kwa kuzaliwa mtanzania
Nyumbani kwetu pazuri wageni
Wanang'ang'ania
Nguo zetu za asili tukivaa tunavutia
Nyimbo zetu ni mwanana tukiimba
Ndege wanashangilia
Watoto wanafurahia
Ninajivunia mimi kuwa mtanzania
Na kiswahili changu ndio ninaringia.
Bendera yetu ya taifa, wimbo wa taifa
Mqenge wa uhuru, ndio nembo zetu
Afrika na duniani pote
Ndizo zatutambulisha
Tanzania, Tanzania
Nakupenda Tanzania
Zana zetu, mapambo yetu
Kazi ya mikono yetu
Sanaa zetu ni burudani
Na elimu kwa jamii yetu
Tujivunie asili yetu
Mzizi wa utamaduni wetu
Tujivunie sisi kuwa watanzania
Na kiswahili chetu kukiringia.
Zuhura Seng'enge.
04/12/2014.
(Please share, leave a comment)
No comments:
Post a Comment
Please share your thoughts and feelings..